MEI 8 kila mwaka tunakumbuka siku ya kuanzishwa kwa Chama cha Msalaba
Mwekundu kilichoasisiwa na mfanyabiashara Mswisi, Henry Dunant,
kufuatia mapigano ya SELFERINO yaliyotokea wakati wa vita ya
AUSTRIA
dhidi ITALIA na UFARANSA mwaka 1859.
Historia ya chama
Hadi
karne ya 19, hapakuwa na utaratibu rasmi wa MATIBABU na huduma ya
uuguzi kwa wanajeshi walioathirika na majanga ya vita na hasa majeruhi.
Hivyo kama bahati kwa DUNANT alipokuwa akisafiri nchini ITALIA mnamo Juni 24, 1859,
Akiwa njiani kuelekea kuonana na mfalme KAIZARI
wa Ufaransa Napoleon wa III, kwa lengo la kujadili matatizo ya KIBIASHARA yaliyokuwa yakiwatokea nchini Algeria, ambayo kwa
wakati huo Algeria ilikuwa ikimilikiwa na Ufaransa.
Dunant alipofika mji mdogo wa SOLFERINO ilikuwa jioni ya Juni 24, ambapo alishtushwa na hali ya kutisha baada ya kushuhudia Vita ya Solferino.
Vita
hiyo ilikuwa ni moja wapo ya mapigano kati ya Vita ya Austro-Sardinian,
ambapo kwa siku moja, takriban askari 40,000 pande zote mbili walikufa
huku wengine wakiwa wamejeruhiwa. Kwa hali hiyo, Dunant alishtushwa na mateso ya askari waliojeruhiwa na uhaba wa matibabu na huduma za kimsingi.
Anatupilia
mbali madhumuni ya hapo awali ya safari yake na kwa siku kadhaa
akajitolea kusaidia katika matibabu na kuwauguza waliojeruhiwa. Anafanikiwa
kupanga msaada wa dharura kwa kuwahamasisha wakazi kutoa misaada bila
ubaguzi. Anaporudi kwao mjini GENEVA, anaandika kitabu kiitwacho ‘A
Memory of Solferino’.
Katika
kitabu hicho aliweza kuandika mambo mbalimbali ikiwemo kubuniwa kwa
mikataba ya kimataifa kuhakikisha ulinzi wa madaktari wasioegemea upande
wowote wa hospitali katika maeneo ya vita ili kusaidia askari
waliojeruhiwa vitani.
Februari 9, 1863, Dunant akiwa mjini Geneva, aliungana na raia wengine 5 na kuanzisha kamati maalum ya kusaidia waathirika wa vita iliyofahamika kama tume ya uchunguzi ya Geneva Society for Public Welfare.
Wajumbe
hao ni
- Gustave Moynier,(mwanasheri),
- Louis Appia (Daktari),
- Theodore Maunoir(Daktari) na
- Guillaume Henri Dufour (Jenerali wa Jeshi la Uswisi).
Siku
nane baadaye, kamati hiyo inaamua kubadili jina la kamati na kuanza
kujulikana kama Kamati ya Kimataifa ya Kutoa Misaada kwa waliojeruhiwa
wakati wa Vita (International Committee for Relief to the Wounded). Kamati hiyo kwa sasa inajulikana kama Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (International Committeee of the Red Cross-ICRC).
Mwaka 1864) serikali
ya Uswisi ilipitia Mkataba wa Geneva na kuboresha hali ya askari ,
majeruhi katika eneo la vita na mataifa hayo yote yalitiliana saini.
Mkutano
huo pia ulibainisha masharti mawili maalum ambayo yangelitambulisha
shirika la kitaifa la kutoa misaada kwa kamati ya kimataifa ambapo
shirika hilo la kitaifa lazima litambuliwe na serikali ya taifa kama
shirika la kutoa misaada kulingana na mkataba huo.
Matumizi
ya alama ya Msalaba Mwekundu yalianza kutumika kwa mara ya kwanza
kwenye vita ya Dybbøl (Denmark) mwaka 1864, kufuatia mgogoro wa silaha
kati ya nchi hizo ambapo Louis Appia na Charles van de Velde, kapteni
katika jeshi la Uholanzi walikuwa wajumbe wa kwanza wasioegemea upande
wowote kufanya kazi chini ya Msalaba Mwekundu katika vita hiyo.
Mwaka 1876, kamati ilijipa jina la ‘Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu’ (ICRC) ambalo ndilo jina lake rasmi hadi hivi sasa. Miaka mitano baadaye, Shirika la Msalaba Mwekundu la Marekani lilianzishwa kwa juhudi za Clara Barton. Nchi
zaidi zilitia saini mkataba wa Geneva na kuanza kuuheshimu kwa uhalisi
wakati wa vita na katika muda mfupi tu, Shirika la Msalaba Mwekundu
lilipata kasi kubwa kama shirikisho la kuheshimika kimataifa.
Tuzo
ya Amani ya Nobel ilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1901, Kamati ya
Nobel ya Norway iliamua kumtuza Henry Dunant pamoja na Frédéric Passy,
mwanaharakati wa kimataifa. Mwaka 1906, mkataba wa Geneva wa 1864 uliundwa upya kwa mara ya kwanza na baadaye
mkataba wa Hague X, ulioratibiwa katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa
Amani mjini Hague, ulipanua mkataba wa Geneva kujumuisha pia vita ya
majini.
Muda
mfupi kabla ya Vita Kuu vya Kwanza vya Dunia kuanza mwaka wa 1914, na
miaka 50 baada ya kuanzishwa kwa ICRC na kupitishwa kwa mkataba wa
Geneva, tayari kulikuwa na vyama vya kitaifa 45 duniani kote.
Mnamo
Oktoba 15, 1914 punde tu baada ya kuanza kwa vita, ICRC ilianzisha
uwakala wake wa kimataifa kwa wafungwa wa vita (POW), ambao walikuwa
1,200 wengi wao wakiwa wafanyakazi wa kujitolea kabla ya mwisho wa
1914. Mnamo
Desemba 10, 1963, shirikisho hili pamoja na ICRC zilipokea tuzo ya
Amani ya Nobel na mwaka 1983, shirikisho lilibadili jina na kuitwa ‘Ligi
ya Vyama vya Msalaba na Hilali Nyekundu’ kuonyesha kuongezeka kwa idadi
ya vyama vya kitaifa chini ya Chama cha Hilali Nyekundu.
Jina
la ligi lilibadilishwa tena mwaka wa 1991 na kuwa rasmi la ‘Shirikisho
la kimataifa la Msalaba Mwekundu na vyama vya Hilali Nyekundu’. Siku hii ya Chama cha Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu ilisherekewa kwa mara ya kwanza duniani kote Mei 8, 1948. Tokea hapo, mwaka 1953, siku ya Msalaba Mwekundu duniani imekuwa ikilenga kila mwaka kwa ujumbe unaohusu kazi za chama hicho duniani.
Mwaka
wa 1997, ICRC na shirikisho zilitia saini mkataba wa Seville ambao
uliainisha majukumu ya mashirika ndani ya muungano ambao uligawanywa
sehemu kuu 3. Muungano huo ni Kamati ya Kimataifa
ya Msalaba Mwekundu (ICRC), Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya
Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) na vyama vya kitaifa vya
Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (NATSOC). Kwa jumla, kuna watu milioni 97 duniani kote ambao hutumikia ICRC, Shirikisho la kimataifa na vyama vya kitaifa.
Henry Dunant Young
Kanuni saba za msingi
Kongamano
la kimataifa la 1965 mjini Vienna liliratibisha kanuni saba za msingi
ambazo zilifaa kutumiwa na pande zote za muungano na ziliongoza kwa
masharti rasmi ya muungano mwaka 1986. Kanuni hizo ni
- UBINADAMU,
- KUTOPENDELEA,
- KUTOEGEMEA UPANDE WOWOTE,
- UHURU,
- KAZI YA KUJITOLEA,
- UMOJA NA UJUMUIYA.

